top of page

Katika Uwanja wa Flander

Katika uwanja wa Flander, maua ya popi hupiga,
Katikati ya misalaba, safu kwa safu,
Ambayo huashiria mahali petu, na pia kwenye anga,
Ndege wa larki, bado huimba kwa ujasiri, huruka
Wakiskika kwa umbali kati ya milipuko ya bunduki.

Sisi ndio wafu, Siku chache zilizopita,
Tuliishi, tukahisi alfajiri, tukaona jua likiwaka,
Tulipenda na kupendwa, na sasa tumelala,
Katika uwanja wa Flander.

Chukua ugomvi wetu na adui,
Kwako kutoka kwa mikono iliyoshindwa tunatupa,
Tochi, iwe yako uishikilie juu,
Kama utavunja imani nasi tunaokufa,
Hatutalala, ingawa maua ya popi yanamea,
Katika uwanja wa Flander.

Translated by Grace M. Kioko, Joshua S. Bichanga

bottom of page